Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 9 Agosti 2018

Waziri wa elimu aipongeza Temeke kwa ujenzi wa shule mpya kata ya Kilung...

Temeke mshindi wa kwanza maadhimisho ya Nanenane kanda ya Mashariki na Pwani.



Temeke yashika nafasi ya kwanza katika maadhimisho ya 25, ya maonesho ya wakulima, wavuvi na wafugaji maarufa kama Nanenane, yaliyoadhimishiwa mkoani Morogoro yakihusisha Kanda ya Mashariki na Pwani.

Huku nafasi ya pili ikishikwa na Kinondoni na yatatu ikienda kwa Ilala.
Aidha Temeke imekua ya pili kwa kanda nzima wakati nafasi ya kwanza imechuliwa na chuo kikuu cha Sua.

Akifunga maonesho hayo, Waziri wa Mifugo Mh: Luhanga Mpina amesema lengo la maadhimisho haya pamoja na kauli mbiu yake ni kuipa thamani sekta hii muhimu ya kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo ndio msingi pekee kuelekea kutekeleza sera ya uchumi wa Kati wa viwanda.

Maadhimisho hayo yaliyoenda kwa kauli mbiu isemayo “Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa Maendeleo ya viwanda” yakilenga kutekeleza sera ya Uchumi wa kati wa viwanda, kwa kanda ya mashariki, yameshirikisha Halmashauri za Mkoa wa Pwani, Dar es Salaam, Morogoro na Tanga.
Temeke ni moja ya Halmashauri ambayo inamuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Dr John Pombe Magufuli katika sera ya Uchumi wa kati wa viwanda kwa vitendo.

Katika mashindano hayo Temeke ilionesha ubunifu wa tofauti kwa kuwashirikisha wajasiriamali kutoka TASAF na wamiliki wa kiwanda kidogo cha viatu ambao walikua kivutio kikubwa kwa namna walivyo zipa thamani bidhaa zao.

Hongera Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Ndg: Nassib Mmbagga kwa juhudi zako katika kuthamini juhudi za kila idara.

Kweli Temeke ni mfano wa kuigwa.




Ijumaa, 3 Agosti 2018

Temeke ya ng'aa Maonesho Nanenane



“Temeke mmejipanga sana, nimejifunza mengi na nimevutiwa na kila kitu nilichokikuta hapa. Hongereni kwa ubunifu” Godwin Sakaya. ni maneno ya mmoja wa wageni aliyehudhuria katika banda letu la Manispaa.

Ikiwa ni moja kati ya washiriki katika maonesho ya wakulima na wafugaji ya  mwaka 2018 katika mji wa Morogoro ambapo maonesho haya yanafanyikia hapa kwa Kanda ya Mashariki na Pwani. Kanda ambayo inajumuisha mikoa ya  Pwani, Dar es Salaam, Tanga na Morogoro.

Temeke kati ya Halmashauri 6 zilizopo katika jiji la Dar es Salaam imejipanga kuwapa wanachi huduma zilizo bora katika msimu huu wa nanenane. Chini ya uongozi makini wa mkurugenzi wake ndg:Nassibu Mmbagga Temeke imeweza kuiishi kauli mbiu ya Mh:Rais,na kuhakikisha tunawekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi ili kuelekea katika uchumi wa viwanda. Hili limedhibitika wazi katika maonesho haya.

Moja ya huduma inayotolewa ni shamba darasa ambalo wataalamu wamekua wakitoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora na namna ya kuandaa shamba lako. Darasa hili limekua msaada sana kwa wakulima wapya ambao wameonesha nia ya dhati katika kuwekeza katika kilimo.

Aidha madaktari bingwa wa kilimo wanatoa huduma ya zahanati ya afya ya mimea, ambayo inatibu mimea iliyo athirika na magonjwa mbalimbali.
Banda la temeke limezungukwa na vipando vingi ikiwemo mboga mbalimbali, kilimo cha viungo (spices) za chakula na dawa, madawa ya asili ya kuzuia wadudu na magonjwa mbalimbali shambani.





Pamoja na hayo kivutio kikubwa katika banda la temeke ni kiwanda cha kutengeneza viatu. Pindi ufikapo katika banda letu utapata fursa ya kujua namna viatu vinavyotengenezwa. Pia utapata kiatu cha aina yako na ukubwa unaotaka.
Kiwanda hiki kinatengeneza bidhaa zote zitokanazo na mifugo kwa kutumia ngozi halisi. Mfano viatu vya aina zote, mikanda na mikoba. Kiwanda hiki ni tafsri tosha kuwa Temeke sasa tumeamua kuwekeza katika Tanzania ya viwanda.



Kama ilivyo shauku ya Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Mh: John Pombe Magufuli kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kujinyanyua kiuchumi hadi kufikia uchumi wa kati, katika kulitekeleza hilo kupitia mpango wa nchi katika kuwasaidia walengwa wa kaya maskini yaani TASAF Temeke imeweza kuwafundisha na kuwasimamia wajasiliamali kupitia mpango huo kwa fedha wanayoipokea kila baada ya miezi miwili. Ambayo wajasiliamali hao wameunda vikundi vya VICOBA ili kujisimamia katika matumizi ya fedha hizo.



Hivyo wajasiliamali hao wapo katika maonesho haya ili kuonesha ubunifu mbalimbali ambao wanaufanya kama usindikaji wa vyakula, mboga na matunda katika viwango vya hali ya juu, ubunifu wa kutumia mikono, na uchakataji wa samaki.

Hakika ukifika katika banda letu la temeke hutatoka bure, kuna mambo mengi mazuri yenye kuvutia.



Maonesho ya nanenane yanaendelea katika viwanja hivi vya Nanenane Morogoro mpaka kufikia kilele chake siku ya tarehe 8/8/2018.

 Kauli mbiu ya mwaka huu ni “wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda”.

Magazeti ya Leo

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 04/08/2018


LINK:  www.temekemc.go.tz

Yaliomo ndani ya banda la Temeke Nanenae Morogoro.

Alhamisi, 2 Agosti 2018

Karibu uone maajabu banda la Temeke kwenye maonesho Nanenane Morogoro.

Tanzia


“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mh:Kassid Seleman Likacha Diwani wa Viti maalum nimeshtuka sikutegemea wala kuwaza maneno aliyoniambia kuwa leo tarehe 27/07/2018 kuwa nisisafiri wala kutoka nje ya Jiji badala yake nikamchukue nimpeleke hospitali”.


Marehemu Mh; Kassid enzi za uhai wake.

Haya ni maneno aliyoyasema Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mh. Abdallah Chaurembo kwa masikitiko makubwa wakati wa kutoa salamu za pole kwa wafiwa na kufanya umati wa waheshiwa Madiwani pamoja na wakuu wa idara kushindwa kujizuia na kutoa machozi wakati wa dua ya kumuombea marehemu ilipokuwa ikifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Idd Nyundo katika Manispaa ya Temeke.



                                  Mwili wa Mh:Kassid ukiwa katika ukumbi wa Iddi Nyundo ili kuagwa. 

Akimuelezea marehemu, alibainisha kuwa alikuwa mtu wa watu anaetambua wajibu wake na kubwa zaidi ambalo litaacha pengo ni ile hali ya kuwa mpatanishi pindi panapoitajika ndani ya Chama cha Mapinduzi ama nje ya chama.
Mh:Kassid ni mtu wa watu hana makuu, ni mchapakazi anaejitambua na kutambua wajibu wake kwa serikali na kwa wananchi anaowahudumia.Nimeguswa sana na msiba huu kwakuwa siku chache zilizopita tulipatwa na msiba mwingine wa Diwani wa viti maalum katika Manispaa ya Kigamboni ambao ni majirani zetu kabisa.


      Pichani marehemu enzi za uhai wake akiwa katika kutekeleza majukumu yake.


Akisoma wosia wa marehemu,walibainisha kuwa marehemu Kassid akizaliwa tarehe 26/06/1969 na alibahatika kupata elimu ya Msingi na Sekondari pia alikuwa mjuzi katika fani ya biashara na ujasiriamali.
Pamoja na hayo katibu Tawala wa Wilaya ndug:Hashim Komba alisema Mh:Kassid ameacha pigo kubwa sana katika chama cha Mapinduzi na kamwe hawezi kutoka katika fikra kutokana na kujituma kwa wakati wote katika majukumu yake.

“Nina uchungu usio na kifani, kwani wiki chache za nyuma nilikwa nae katika majukumu ya kazi na tulipanga mikakati mingi ya kimaendeleo na kuahidi kulinda heshima ya Chama na kupiga hatua mbele zaidi ,kumbe Mungu anamipango mingi kuliko wanadamu, leo Kassid umelala hutaamka tena ila naahidi nitalinda na kutimiza mambo yote ya kazi tuliyokubaliana na kuyapanga” alisema Komba.

Marehemu alikuwa Diwani wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi tangu mwezi Oktoba 2015 hadi mauti ilipomfika tarehe 26/07/2018 katika Hospitali ya Temeke alipokuwa akipatiwa matibabu.









Jumatano, 1 Agosti 2018

Tanzia


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anasikitika kutangaza kifo cha aliyekua  Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 kilichotokea tarehe 25/07/2018 Ndg: Photidas Kagimbo.
Kilichotekea katika hospitali ya taifa muhimbili.




"Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amen"

Temeke mpya kufikia 2020.

Tanzia


TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...