“Temeke mmejipanga
sana, nimejifunza mengi na nimevutiwa na kila kitu nilichokikuta hapa.
Hongereni kwa ubunifu” Godwin Sakaya. ni maneno ya mmoja wa wageni aliyehudhuria
katika banda letu la Manispaa.
Ikiwa ni moja kati
ya washiriki katika maonesho ya wakulima na wafugaji ya mwaka 2018 katika mji wa Morogoro ambapo
maonesho haya yanafanyikia hapa kwa Kanda ya Mashariki na Pwani. Kanda ambayo
inajumuisha mikoa ya Pwani, Dar es
Salaam, Tanga na Morogoro.
Temeke kati ya
Halmashauri 6 zilizopo katika jiji la Dar es Salaam imejipanga kuwapa wanachi
huduma zilizo bora katika msimu huu wa nanenane. Chini ya uongozi makini wa
mkurugenzi wake ndg:Nassibu Mmbagga Temeke imeweza kuiishi kauli mbiu ya Mh:Rais,na
kuhakikisha tunawekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi ili kuelekea katika
uchumi wa viwanda. Hili limedhibitika wazi katika maonesho haya.
Moja ya huduma
inayotolewa ni shamba darasa ambalo wataalamu wamekua wakitoa elimu kwa
wananchi juu ya kilimo bora na namna ya kuandaa shamba lako. Darasa hili
limekua msaada sana kwa wakulima wapya ambao wameonesha nia ya dhati katika kuwekeza
katika kilimo.
Aidha madaktari
bingwa wa kilimo wanatoa huduma ya zahanati ya afya ya mimea, ambayo inatibu
mimea iliyo athirika na magonjwa mbalimbali.
Banda la temeke limezungukwa
na vipando vingi ikiwemo mboga mbalimbali, kilimo cha viungo (spices) za
chakula na dawa, madawa ya asili ya kuzuia wadudu na magonjwa mbalimbali
shambani.
Pamoja na hayo
kivutio kikubwa katika banda la temeke ni kiwanda cha kutengeneza viatu. Pindi
ufikapo katika banda letu utapata fursa ya kujua namna viatu vinavyotengenezwa.
Pia utapata kiatu cha aina yako na ukubwa unaotaka.
Kiwanda hiki
kinatengeneza bidhaa zote zitokanazo na mifugo kwa kutumia ngozi halisi. Mfano
viatu vya aina zote, mikanda na mikoba. Kiwanda hiki ni tafsri tosha kuwa
Temeke sasa tumeamua kuwekeza katika Tanzania ya viwanda.
Kama ilivyo shauku
ya Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Mh: John Pombe Magufuli kuhakikisha kila
mwananchi anapata fursa ya kujinyanyua kiuchumi hadi kufikia uchumi wa kati, katika
kulitekeleza hilo kupitia mpango wa nchi katika kuwasaidia walengwa wa kaya
maskini yaani TASAF Temeke imeweza kuwafundisha na kuwasimamia wajasiliamali
kupitia mpango huo kwa fedha wanayoipokea kila baada ya miezi miwili. Ambayo
wajasiliamali hao wameunda vikundi vya VICOBA ili kujisimamia katika matumizi
ya fedha hizo.
Hivyo wajasiliamali
hao wapo katika maonesho haya ili kuonesha ubunifu mbalimbali ambao wanaufanya
kama usindikaji wa vyakula, mboga na matunda katika viwango vya hali ya juu,
ubunifu wa kutumia mikono, na uchakataji wa samaki.
Hakika ukifika
katika banda letu la temeke hutatoka bure, kuna mambo mengi mazuri yenye
kuvutia.
Maonesho ya nanenane
yanaendelea katika viwanja hivi vya Nanenane Morogoro mpaka kufikia kilele
chake siku ya tarehe 8/8/2018.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “wekeza katika
kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni