Temeke yashika nafasi ya
kwanza katika maadhimisho ya 25, ya maonesho ya wakulima, wavuvi na wafugaji maarufa
kama Nanenane, yaliyoadhimishiwa mkoani Morogoro yakihusisha Kanda ya Mashariki
na Pwani.
Huku nafasi ya pili ikishikwa
na Kinondoni na yatatu ikienda kwa Ilala.
Aidha Temeke imekua ya
pili kwa kanda nzima wakati nafasi ya kwanza imechuliwa na chuo kikuu cha Sua.
Akifunga maonesho hayo,
Waziri wa Mifugo Mh: Luhanga Mpina amesema lengo la maadhimisho haya pamoja na
kauli mbiu yake ni kuipa thamani sekta hii muhimu ya kilimo, Mifugo na Uvuvi
ambayo ndio msingi pekee kuelekea kutekeleza sera ya uchumi wa Kati wa viwanda.
Maadhimisho hayo
yaliyoenda kwa kauli mbiu isemayo “Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa
Maendeleo ya viwanda” yakilenga kutekeleza sera ya Uchumi wa kati wa viwanda,
kwa kanda ya mashariki, yameshirikisha Halmashauri za Mkoa wa Pwani, Dar es
Salaam, Morogoro na Tanga.
Temeke ni moja ya
Halmashauri ambayo inamuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh:
Dr John Pombe Magufuli katika sera ya Uchumi wa kati wa viwanda kwa vitendo.
Katika mashindano hayo
Temeke ilionesha ubunifu wa tofauti kwa kuwashirikisha wajasiriamali kutoka
TASAF na wamiliki wa kiwanda kidogo cha viatu ambao walikua kivutio kikubwa kwa
namna walivyo zipa thamani bidhaa zao.
Hongera Mkurugenzi Mtendaji
Mkuu Ndg: Nassib Mmbagga kwa juhudi zako katika kuthamini juhudi za kila idara.
Kweli Temeke ni mfano wa
kuigwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni