“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha
Mh:Kassid Seleman Likacha Diwani wa Viti maalum nimeshtuka sikutegemea wala
kuwaza maneno aliyoniambia kuwa leo tarehe 27/07/2018 kuwa nisisafiri wala
kutoka nje ya Jiji badala yake nikamchukue nimpeleke hospitali”.
Marehemu Mh; Kassid enzi za uhai wake.
Haya ni maneno aliyoyasema Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Temeke Mh. Abdallah Chaurembo kwa masikitiko makubwa wakati wa kutoa salamu za
pole kwa wafiwa na kufanya umati wa waheshiwa Madiwani pamoja na wakuu wa idara
kushindwa kujizuia na kutoa machozi wakati wa dua ya kumuombea marehemu
ilipokuwa ikifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Idd Nyundo katika Manispaa ya
Temeke.
Mwili wa Mh:Kassid ukiwa katika ukumbi wa Iddi Nyundo ili kuagwa.
Akimuelezea marehemu, alibainisha kuwa alikuwa mtu wa watu anaetambua wajibu wake na kubwa zaidi ambalo litaacha pengo ni ile hali ya kuwa mpatanishi pindi panapoitajika ndani ya Chama cha Mapinduzi ama nje ya chama.
Mh:Kassid ni mtu wa watu hana makuu, ni mchapakazi
anaejitambua na kutambua wajibu wake kwa serikali na kwa wananchi
anaowahudumia.Nimeguswa sana na msiba huu kwakuwa siku chache zilizopita
tulipatwa na msiba mwingine wa Diwani wa viti maalum katika Manispaa ya
Kigamboni ambao ni majirani zetu kabisa.
Pichani marehemu enzi za uhai wake akiwa katika kutekeleza majukumu yake.
Akisoma wosia wa marehemu,walibainisha kuwa marehemu Kassid akizaliwa tarehe 26/06/1969 na alibahatika kupata elimu ya Msingi na Sekondari pia alikuwa mjuzi katika fani ya biashara na ujasiriamali.
Akisoma wosia wa marehemu,walibainisha kuwa marehemu Kassid akizaliwa tarehe 26/06/1969 na alibahatika kupata elimu ya Msingi na Sekondari pia alikuwa mjuzi katika fani ya biashara na ujasiriamali.
Pamoja na hayo katibu Tawala wa Wilaya ndug:Hashim Komba
alisema Mh:Kassid ameacha pigo kubwa sana katika chama cha Mapinduzi na kamwe
hawezi kutoka katika fikra kutokana na kujituma kwa wakati wote katika majukumu
yake.
“Nina uchungu usio na kifani, kwani wiki chache za nyuma
nilikwa nae katika majukumu ya kazi na tulipanga mikakati mingi ya kimaendeleo
na kuahidi kulinda heshima ya Chama na kupiga hatua mbele zaidi ,kumbe Mungu
anamipango mingi kuliko wanadamu, leo Kassid umelala hutaamka tena ila naahidi
nitalinda na kutimiza mambo yote ya kazi tuliyokubaliana na kuyapanga” alisema
Komba.
Marehemu alikuwa Diwani wa viti maalum kwa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi tangu mwezi Oktoba 2015 hadi mauti ilipomfika tarehe 26/07/2018 katika
Hospitali ya Temeke alipokuwa akipatiwa matibabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni