Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 16 Mei 2018

Zaidi ya wakandarasi 100 wanufaika.



Zaidi ya wakandarasi 100 wanufaika na semina ya bure toka National Microfinance Bank (NMB) ya namna ya kushinda zambuni mbalimbali zinazotangazwa hapa nchini.

Akizungumza na wakandarasi  hao katika ukumbi wa Idd Nyundo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndugu Nassib Mmbaga aliwataka wakandarasi hao kutumia nafasi hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ilioyotolewa na kujipatia mikopo ili kuweza kuwa na ushindani pindi fursa zinapotangazwa tenda mbalimbali zinatangazwa wasisite kuomba kwani hiyo ni fursa pekee ya kujitokeza na kuonyesha uwezo katika kazi na kampuni husika.

Nae Meneja wa kanda Ndugu Badru Idd aliwatoa hofu wakandarasi hao na kuwataka wasisite kujitokeza kuomba mikopo na ushauri toka NMB, ili kuweza kuibuka vinara katika soko la ushindani pindi zitangazwapo zabuni mbalimbali.

''NMB ni benki ya kizalendo hivyo msisite kutuona na tufanye mazungumzo ya namna bora ya kusaidiana na kujikwamua kimaisha, mikopo yetu ni rahisi na yenye riba nafuu kwa mwananchi yoyote aliedhamiria kujikomboa. Pia tuna matawi mengi karibu kila mahali hapa Dar es salaam hivyo tumekufikia popote ulipo'' Alisisitiza.



Vile vile alibainisha kwamba ukiwa na NMB unaweza kupata mikopo na huduma zozote za kielektroniki pamoja na mikopo mbalimbali, pia alielezea uwepo wa akaunti mbalimbali za biashara mfano World Wide akaunti, Business Saving akaunti, Fanikiwa akaunti na NMB connect akaunti ambapo zote hizi ni maalumu kwa wafanyabiashara.

Semina hiyo ya siku moja ilifanyika ikiwa na lengo madhubuti la kuwasaidia wakandarasi na kuwatoa hofu ya kuomba mikopo NMB, ili kuwawezesha kushika tenda zinazotangazwa hapa nchini hususani zilizopo ndani ya Manispaa ya Temeke.


Ijumaa, 11 Mei 2018

Temeke kuboresha huduma za Afya 11/05/2018

Wazee wanufaika na vitambulisho vya Afya

Zaidi ya wazee  7,005 wenye umri wa miaka 60 nakuendelea wanufaika na vitambulisho vya matibabu bure katika kata 23 za Manispaa ya Temeke.

Akizindua vitambulisho hivyo Mstahiki Meya Mh.Abdallh Chaurembo aliwataka wazee hao kuvitunza vitambulisho vyao ili pindi watakapohitaji huduma za matibabu iwe rahisi kuhudumiwa kwa kuwa wanatambulika rasmi, pia alisisitiza matumizi ya vitambulisho hivyo ni ndani ya Manispaa ya Temeke tu.



''Serikali yetu inawajali sana wazee na kwa kuliona hilo imeamua kutengeneza vitambulisho vya matibabu ya afya ili kuhakikisha mnapata huduma hizo kwa urahisi na kwa kupewa vipaombele,hivyo basi mvitunze na kuhakikisha mnavibeba kila mnapoenda kupata matibabu'' alisisitiza.

Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr Gwamaka akielezea zoezi hili alisema ''utambuzi wa wazee ulianza tangu tarehe 27/09/2017 na kufanikiwa kutambua wazee 10,879 katika kata 23 za Manispaa ambapo wanawake waliotambuliwa ni 5220 na wanaume 5659''.

Vilevile alibainisha tiba kwa kadi(TIKA) itaanza muda si mrefu ambayo mlengwa atapata matibabu ndani ya mkoa  husika na kwa kila kaya ni 150,000/= na kwa mtu mmoja ni 40,000/=tu.



Mpango wa utengenezaji  wa vitambulisho vya wazee unaratibiwa chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa kuhakikisha inawapa vipaombele vya matibabu, kata zilizonufaika na zoezi hili ni kata ya Mtoni 564, Tandika 703, Azimio 583,Buza 624, Miburani 411, Keko 355, Tandika 703, Azimio 583, Temeke Hospital  451, Yombo vituka  668, Chang'ombe 490, Temeke 575 na Mbagala 674, Vyote vipo ndani ya Manispaa ya Temeke.

Jumatatu, 7 Mei 2018

Wataalamu wa afya waendelea kupata mafunzo juu ya mfumo wa CHF



Pichani mafunzo ya watendaji ngazi ya Halmashauri wakitoa mafunzo ya  DHFF, FFARS, CHF iliyoboreshwa na mfumo wa JAZIA(PVS) kwa waganga wafawidhi,wahasibu,makatibu ,phamasia  na wenyeviti wa bodi na wajumbe wake kutoka zahanati zote za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.


Mafunzo haya ni mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika kwa wataalamu wa afya katika ngazi ya Manispaa ambayo yalidumu kwa siku tatu na kuzinduliwa na  Katibu Tawala Mkoa Bib. Theresia Mmbando.



Mafunzo hayo yenye lengo la uelewa mpana wa maana ya ugatuaji wa mipango ya Afya na bajeti kwa utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma(DHFF) yenye matarajio ya kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa uandaaji wa mipango, bajeti na matumizi yanayolenga kuboresha huduma za Afya.



Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Wizara ya afya pamoja na wadau wengine wa elimu wameamua kuboresha utoaji wa huduma za afya.



Kila la Kheri Kidato cha Sita



Baraza la Madiwani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wanawatakia mitihani mema kwa watahiniwa wote wa kidato cha sita katika mitihani yao iliyoanza leo tarehe 07/05/2018.

Jumla ya watahiniwa 2230 watafanya mitihani ya kidato cha sita katika wilaya ya Temeke. Ambapo 1840 ni watahiniwa wa shule na 390 ni watahiniwa wa kujitegemea.

Mitihani itasambazwa katika shule 15 na vituo 2 . Mitihani hiyo ya kidato cha sita inatarajiwa kamalizika tarehe 16/05/2018.  


Ijumaa, 4 Mei 2018

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA WAKUFUNZI KATIKA NGAZI YA WILAYA ITAKAYOLENGA MASUALA YA DHFF, FFARS, CHF ILIYOBORESHWA NA MFUMO WA JAZIA(PVS)





Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imefanya ufunguzi wa mafunzo ya mifumo ya afya iliyoboreshwa.Mafunzo haya yalianzia ngazi ya kitaifa,Mkoa na sasa ni ngazi ya Wilaya na baada ya mafunzo haya taaluma hii itapelekwa ngazi ya vituo vya afya.
Akifungua uzinduzi huo Katibu Tawala wa Mkoa Bibi. Theresia Mmbando aliwapongeza Wizara ya Afya kwa kuandaa mafunzo yenye tija katika sekta ya Afya. kwani mafunzo haya yatasaidia kupunguza urasimu na kuboresha huduma za afya.

Mmbando alisema '' lengo mahususi la mafunzo hayo kuwa ni uelewa mpana wa maana ya ugatuaji wa mipango ya Afya na bajeti kwa utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma(DHFF) yenye matarajio ya kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa uandaaji wa mipango, bajeti na matumizi yanayolenga kuboresha huduma za Afya''.

Alifafanua zaidi mafunzo hayo yamedhamiria kuwajengea uwezo watendaji wa ngazi ya mamlaka za Serikali za mitaa. watendaji wa ngazi ya jamii, ambapo watendaji hao watakuwa wawekezaji katika vituo vya kutolea huduma za Afya. Lengo kuu ni kutekeleza hatua za kuboresha huduma za afya kupitia utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo , utekelezaji wa CHF iliyoboreshwa pamoja na mfumo wa wa kutumia MSHITIRI/JAZIA (Prime Vendor-PVS).
Maboresho haya yatasaidia  manunuzi ya dawa , vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pale vinapokosekana kutoka  Bohari  kuu ya dawa(MSD).

Aliwashukuru pia wadau wa maendeleo kwa kukubali kuendesha semina katika ngazi za Halmashauri ,Vituo vya kutolea huduma pamoja na ngazi ya jamii.
Akizungumza na washiriki  katika semina hiyo Dr. Mariam Ongara toka Wizara ya Afya amesema kumekuwa na changamoto mbalimbali katika uendeshaji na utoaji wa huduma katika maeneo mengi nchini hivyo kuifanya serikali kuchukua hatua na kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiuendeshaji ili kukabiliana na changamoto hizo.

Vilevile alizungumzia mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya Afya uliofanyika Dec 7,2016 iliamua kuanzisha utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuzipa nguvu zaidi kamati za usimamizi wa huduma za afya(HFGC) katika kupanga na kusimamia huduma za afya katika ngazi ya jamii.

Utekelezaji wa mkakati huu unalenga kugatua madaraka ya uendeshaji wa huduma za afya katika ngazi za vituo ili kupunguza urasimu na kuboresha utoji wa huduma za afya. Katika kukabiliana na changamoto hizo serikali kwa kushirikiana na wadau imeamua kutekeleza mfumo wa CHF iliyoboreshwa ambao umekuwa ukitekelezwa katika mikoa mitatu ya Dodoma Morogoro na Shinyanga ndani ya miaka mitano chini ya mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS)kwa mafanikio.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Iddi Nyundo  Manispaa ya Temeke. watendaji zaidi ya 50 watapata mafunzo kutoka kwa wadau wa mfuko wa Afya wa pamoja(Health Basket Fund), HPSS, PS3, Global Supply Chain Program, Boresha Afya Deloitte, World Vision,EGPAF, Jhpiego, GIZ,AGPAHI na Pharmacies.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...