Pichani mafunzo ya watendaji
ngazi ya Halmashauri wakitoa mafunzo ya DHFF, FFARS, CHF iliyoboreshwa na mfumo wa JAZIA(PVS)
kwa waganga wafawidhi,wahasibu,makatibu ,phamasia na wenyeviti wa bodi na wajumbe wake kutoka
zahanati zote za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Mafunzo haya ni
mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika kwa wataalamu wa afya katika ngazi ya Manispaa
ambayo yalidumu kwa siku tatu na kuzinduliwa na Katibu Tawala Mkoa Bib. Theresia Mmbando.
Mafunzo hayo yenye
lengo la uelewa mpana wa maana ya ugatuaji wa mipango ya Afya na bajeti kwa
utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma(DHFF)
yenye matarajio ya kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa
uandaaji wa mipango, bajeti na matumizi yanayolenga kuboresha huduma za Afya.
Manispaa ya Temeke
kwa kushirikiana na Wizara ya afya pamoja na wadau wengine wa elimu wameamua
kuboresha utoaji wa huduma za afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni