Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 11 Mei 2018

Wazee wanufaika na vitambulisho vya Afya

Zaidi ya wazee  7,005 wenye umri wa miaka 60 nakuendelea wanufaika na vitambulisho vya matibabu bure katika kata 23 za Manispaa ya Temeke.

Akizindua vitambulisho hivyo Mstahiki Meya Mh.Abdallh Chaurembo aliwataka wazee hao kuvitunza vitambulisho vyao ili pindi watakapohitaji huduma za matibabu iwe rahisi kuhudumiwa kwa kuwa wanatambulika rasmi, pia alisisitiza matumizi ya vitambulisho hivyo ni ndani ya Manispaa ya Temeke tu.



''Serikali yetu inawajali sana wazee na kwa kuliona hilo imeamua kutengeneza vitambulisho vya matibabu ya afya ili kuhakikisha mnapata huduma hizo kwa urahisi na kwa kupewa vipaombele,hivyo basi mvitunze na kuhakikisha mnavibeba kila mnapoenda kupata matibabu'' alisisitiza.

Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr Gwamaka akielezea zoezi hili alisema ''utambuzi wa wazee ulianza tangu tarehe 27/09/2017 na kufanikiwa kutambua wazee 10,879 katika kata 23 za Manispaa ambapo wanawake waliotambuliwa ni 5220 na wanaume 5659''.

Vilevile alibainisha tiba kwa kadi(TIKA) itaanza muda si mrefu ambayo mlengwa atapata matibabu ndani ya mkoa  husika na kwa kila kaya ni 150,000/= na kwa mtu mmoja ni 40,000/=tu.



Mpango wa utengenezaji  wa vitambulisho vya wazee unaratibiwa chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa kuhakikisha inawapa vipaombele vya matibabu, kata zilizonufaika na zoezi hili ni kata ya Mtoni 564, Tandika 703, Azimio 583,Buza 624, Miburani 411, Keko 355, Tandika 703, Azimio 583, Temeke Hospital  451, Yombo vituka  668, Chang'ombe 490, Temeke 575 na Mbagala 674, Vyote vipo ndani ya Manispaa ya Temeke.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...