Baraza la Madiwani na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wanawatakia mitihani mema kwa watahiniwa wote
wa kidato cha sita katika mitihani yao iliyoanza leo tarehe 07/05/2018.
Jumla ya watahiniwa 2230 watafanya mitihani ya kidato cha sita katika wilaya ya Temeke. Ambapo 1840 ni watahiniwa wa shule na 390 ni watahiniwa wa kujitegemea.
Mitihani itasambazwa katika shule 15 na vituo 2 . Mitihani hiyo ya kidato cha sita inatarajiwa kamalizika tarehe 16/05/2018.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni