Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 29 Machi 2018

MEYA ZANZIBAR AFURAHISHWA NA UTENDAJI TEMEKE


Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa ya Mjini Zanzibari Mh; Khatibu Abdulrahman afurahishwa na juhudi za uwendezeshwaji wa shughuli za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Alisema hayo wakati wa kuhitimisha mafunzo yaliyodumu ndani ya siku tatu katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo Manispaa ya Temeke.




Abdulrahman alionesha utayari wa kufanya mabadiliko katika halmashauri ya Zanzibari baada ya kupata mafunzo hayo. Pia aliwapongeza uongozi mzima wa Manispaa ya Temeke kwa jinsi walivyojipanga kuhakikisha wanawafikia wananchi katika nyanja zote za kijamii.
Mafunzo hayo ambayo yalifungwa na Mstahiki Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo,alisema ''mafunzo haya yatadumisha ukaribu na mahusiano ya utendaji wa  halmashauri zetu hivyo tuendeleze''. aliwapongeza wageni kwa kuja na kujifunza kwetu, na pia aliwakaribisha wakati mwingine kuja kujifunza Temeke.    





LYANIVA KUTATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA TANDIKA


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva aongea na wafanyabiashara wa Tandika na kuwaahidi kutatua kero zinazowapata pindi wawapo katika biashara zao. Aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea maeneo yanayotoa huduma za jamii katika wilaya ya Temeke. Lyaniva aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa ataondoa kero zote zinazolikumba soko hilo . Moja ya kero kubwa inayoikumba soko hilo ni miundo mbinu inayoizunguka soko hilo, ikiwemo kutuama kwa maji kipindi cha mvua. Lyaniva awaahidi kuwa atashughulikia kero hizo ili kuhakikisha mahali hapo panakua salama kwaajili ya kutoa huduma za kijamii.




Katika ziara hiyo aliambatana na katibu Tawala wilaya,watumishi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,diwani wa Tandika,wenyeviti wa Mitaa,wakuu wa vyama vya siasa mbalimbali,wajumbe wa Mitaa,afisa Tarafa Chang'ombe na wadau wa utoaji huduma za jamii mbalimbali ikiwemo TARURA,TAKUKURU,DAWASCO na TRA.
Katika hatua ingine mkuu wa wilaya alielekea ofisi ya kata ya Tandika ambapo alifanya kikao cha wadau wa maendeleo na wananchi. Ambapo alisisitiza kuhakikisha wanafunzi wote waliofauru darasa la saba 2017 kama wameripoti shuleni. Aliwaasa wazazi kutoa ushirikiano ili watoto wao wasibaki nyumbani kujiingiza katika makundi hatarishi.
Hata hivyo Lyaniva aliwataka wananchi kutoa kiwango stahiki cha kuzoa takataka ili kusaidia zoezi la ukusanyaji taka kuwa rahisi. Pia alisisitiza usafi wa kila jumamosi kwa wananchi wote ni lazima.
Pia aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo ya jamii inayotolewa na serikali kwa riba nafuu kupitia benki ya DCB. Wakinamama na vijana wamehamasishwa kwenda kuchangamkia fursa hiyo ili kujikwamua katika hali ya kiuchumi na jamii.
Lyaniva alisisitiza kuwa rushwa ni adui wa haki hivyo endapo mwananchi atakutana na mazingira yoyote ya rushwa atoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU Wilaya ili hatua kali za kisheria zichukuliwe. Alisema huduma za jamii ni bure kwa kila mtu hivyo wananchi wasiruhusu vitendo vya rushwa. Aidha aliwataka wananchi kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ili kuiongezea mapato serikali,na kwa mapato hayo hayo yatasaidia kuboresha huduma za jamii.




Ziara hiyo ya mkuu wa wilaya yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo katika jamii itaendelea katika kata zote zilizopo wilaya ya Temeke katika vipindi tofauti tofauti.







Jumanne, 27 Machi 2018

DMDP YAPANIA KUFANYA MABADILIKO



Timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ikiongozwa na mratibu wa mradi Bw. Edward Simon pamoja na washauri kutoka taasisi mbalimbali na Viongozi wa Serikali za Mitaa wapitia michoro ya barabara na masoko ili kulinganisha na hali halisi ya maeneo yanayohitaji  huduma ya haraka.

 Huduma hizo ni pamoja na barabara na  madaraja ambapo kwa sasa kumekuwa na changamoto ya vivuko  na ubovu miundombinu unaopelekea ucheleweshwaji wa shughuli za kimaendeleo kutokana na kutofikika kwa urahisi, Ubovu huo hupelekea wagonjwa wengi kupoteza maisha  ama kufika katika vituo vya Afya  wakiwa katika hali mbaya.


Maeneo husika yatakayopitiwa na mradi  huu ni pamoja na  Soko la Mtoni Mtongani na Barabara ya TRH, Aljazira, Muungano, Klinic, Kizinga, Ndibalema na Bugdadi.


WATAALAMU WAKIWA KATIKA MAJADILIANO



ENEO LA SOKO




BARABARA YA TRH


Jumatatu, 26 Machi 2018

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MAGARI 181 KATIKA WILAYA YA TEMEKE




Rais John Pombe Magufuli azindua Magari 181 ya kusambaza Dawa na Vifaa Tiba Nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika bohari ya madawa MSD iliyopo katika Wilaya  ya Temeke.
Akieleza kuhusu Sekta ya Afya Nchini Mh Rais alisema ‘’miongoni mwa sekta zinazotengewa fedha nyingi na Serikali ni pamoja na Sekta hii”, Ukilinganisha na kipindi kilichopita Bajeti ya Dawa imeongezwa kutoka Bilioni 31 mpaka kufikia Bilioni 269  ili kuwafikia walengwa katika vituo vyote vya Afya hapa nchini alisisisitiza.
Pia aliwashukuru Global Fund kwa Msaada wao na juhudi walizofanya  hatimae kutupatia msaada wa Magari hayo.Pia aliwataka wazawa wachangamkie fursa ya kuanzisha Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba hapa nchini ili kupunguza gharama za ununuzi , Kwani asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi
Nae Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu alimshukuru Mh Rais kwa kuwekeza kwenye Afya za Watanzania,pia aliweka wazi ‘’asilimia 97 ya watoto wote nchini wanapatiwa chanjo na kuanzia Julai 2017 Serikali ilianza kupeleka fedha za Dawa moja kwa moja kwenye Zahanati na Vituo vya Afya Nchi nzima’’ Alisema.
Pia Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bw Laurean Bwanakunu Alimshukuru Mh Rais Magufuli kwa kuongeza Bajeti ya  Bohari ya Dawa ,Pia alizungumzia magari hayo yana jumla ya thamani ya sh Bilion 20.7na kusisitiza msaada huo kutoka Global Fund hauna masharti yoyote.
Mwaka huu wa Fedha MSD imefanikiwa kuuza madawa yenye thamani ya  sh Bilioni 8,pamoja na uzinduzi huu Serikali ya Zanzibar imekubali kununua Dawa kutoka Bohari ya Dawa .


Jumanne, 13 Machi 2018

MKUU WA WILAYA TEMEKE AHIMIZAKUISHI AMANI NA UMOJA.
























                                             Mkuu wa wilaya Temeke Mhe:Felix Lyaniva

Mkuu wa wilaya Temeke mhe: Felix Lyaniva amewaasa waumini wa dini ya Kiislamu kuepuka migogoro na badala yake waimarishe umoja na udugu ili kuweza kudumisha amani iliyopo katika nchi yetu. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu wa madrassa mbalimbali zilizopo katika wilaya Temeke, katika mkutano ulioandaliwa na baraza la waislamu Tanzania(BAKWATA) wilaya Temeke uliofanyika katika Chuo cha Ualimu (DUCE).


                                     Walimu wa Madrassa waliohudhuria kikao hicho
                                                  
Aidha katika Hadhara hiyo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es salaam Sheikh Alhadi Musa Salim amesema na kuwaasa waumini wa kiislamu na viongozi wake kufuata kauli mbiu ya ya Baraza la waislamu Tanzania (BAKWATA) inayosema Walimu Tujitambue Tubadilike Tuache Mazoea. ili kuweza kutengeneza jamii yenye maadili mema na uadilifu kwa jamii  ya kiislamu na Mkoa kiujumla. Vilevile aliwasisitiza walimu wa madrassa kuwafundisha wanafunzi wao yaliyo mema na kutengeneza mtaala mmoja wa kufundishia masomo ya dini ya kiislamu.

                         Sheikh Mkuu wa Mkoa Wa Dsm Alhadi Musa Salim.
                     
Pamoja hayo wananchi wa wilaya Temeke wanatakiwa kudumisha ulinzi na usalama wa wilaya yao kwani jamii yoyote yenye amani na utulivu ndio huchochea maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.

Ijumaa, 2 Machi 2018

TEMEKE YATOFAUTI


Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imekadiria kukusanya kiasi cha sh. 251.7 kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa mwaka 2018/2019.
Akisoma bajeti hiyo katika kikao cha madiwani Mkurugenzi wa Manispaa Ndg; Naseeb Mmbaga alisema kiasi hicho cha fedha kitapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo makusanyo ya ndani, ruzuku kutoka serikali kuu na wahisani.
Alisema ndani ya kipindi hicho shilingi 219,076,455,243 zitatokana na ruzuku kutoka serikali kuu,  sh.32,377,175,000 zitatokana na vyanzo vya ndani na wahisani sh. 204,017,500.



Alisema tofauti na miaka iliyopita, bajeti ya mwaka hu italenga zaidi miradi katika sekta ya afya,elimu ya sekondari na msingi, miundombinu mbalimbali, mishahara na matumizi mengineyo.






''Lengo la bajeti ya mwaka huu kuona sekta hizi muhimu nilizozitaja zinakuwa kwakasi katika kukabiliana na ongezeko la watu na mahitaji yao ya kila siku'', alisema Mmbaga.
Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo Mstahiki Meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo, aliwataka watendaji na madiwani kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kulipa kodi stahiki ili mipango ya Halmashauri hiyo itekelezwe kwa wakati.




Alisema tayari elimu ya ukusanyaji kodi kwa viongozi hao imetolewa na kilichobaki kufanya kazi kwa nguvu kuhakikisha kila kata inakusanya mapato katika kiwango kinachotakiwa.
''Muda wa kusubiri ruzuku ya serikali kuu ili mipango yetu ya maendeleo iweze kutekelezwa umekiwisha, lazima sisi wenyewe tujitosheleze kifedha na hilo litafanikiwa kama sisi viongozi tutawajibika kuwahimiza wananchi kulipa kodi'' alisema Chaurembo.  






Alhamisi, 1 Machi 2018

TANGAZO KWA UMMA


TANGAZO KWA UMMA


TANGAZO KWA UMMA



TEMEKE NA KASI YA MAENDELEO


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh; Felix Lyaniva awataka wadau wa maendeleo Temeke kuhamasisha ulipaji wa kodi na tozo zinazotozwa na Halmashauri ikiwemo leseni,ushuru na faini mbalimbali.Aliyasema hayo alipokua akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo katika viwanja vya Manispaa Temeke.Kikao hicho kilijumuisha wakuu wa idara na vitengo, watendaji wa kata 23 za Temeke,viongozi wa dini,wawakilishi wa wananchi, viongozi wa vyama vya siasa mbalimbali,makundi maalumu na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Temeke.




Kikao kilijadiri mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019, hivyo wajumbe walipitia na kutoa mawazo yao katika uboreshwaji wa makisio ya bajeti mpya.
Hata hivyo Halmashauri ya manispaa ya temeke kwa kupitia wataalamu wake mbalimbali inatazamia kukusanya zaidi ya Bilioni 32 katika vyanzo vyake vya ndani,ikiwa ni makisio ya bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2018/2019.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inatazamia kutumia Sh;Bilioni 15,452,505,000.00  kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo inagusa jamii kwa ujumla. Miradi inayotazamiwa kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa shule za msingi na sekondari,ununuzi wa madawati, ujenzi wa zahanati,kujenga miundo mbinu ya usambazaji maji na ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na wakala wa barabara TARURA.




Aidha Mkuu wa Wilaya aliwataka watendaji kusimamia utekelezwaji wa bajeti mpya kwa misingi ya haki, na kuongeza ubunifu katika kupatikana vyanzo vipya vya mapato.
Lyaniva aliwakumbusha wajumbe wote kuwa mabalozi wazuri katika nafasi zao za utendaji ili kumunga mkono Raisi wa nchi Mh;John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuleta maendeleo ya kijamii ikiwemo sera ya Elimu bure.

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...