Rais John Pombe Magufuli azindua Magari 181 ya kusambaza Dawa
na Vifaa Tiba Nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika bohari ya madawa MSD
iliyopo katika Wilaya ya Temeke.
Akieleza kuhusu Sekta ya Afya Nchini Mh Rais alisema ‘’miongoni
mwa sekta zinazotengewa fedha nyingi na Serikali ni pamoja na Sekta hii”, Ukilinganisha
na kipindi kilichopita Bajeti ya Dawa imeongezwa kutoka Bilioni 31 mpaka
kufikia Bilioni 269 ili kuwafikia walengwa
katika vituo vyote vya Afya hapa nchini alisisisitiza.
Pia aliwashukuru Global Fund kwa Msaada wao na juhudi
walizofanya hatimae kutupatia msaada wa
Magari hayo.Pia aliwataka wazawa wachangamkie fursa ya kuanzisha Viwanda vya
Dawa na Vifaa Tiba hapa nchini ili kupunguza gharama za ununuzi , Kwani
asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi
Nae Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
Mh Ummy Mwalimu alimshukuru Mh Rais kwa kuwekeza kwenye Afya za Watanzania,pia
aliweka wazi ‘’asilimia 97 ya watoto wote nchini wanapatiwa chanjo na kuanzia
Julai 2017 Serikali ilianza kupeleka fedha za Dawa moja kwa moja kwenye
Zahanati na Vituo vya Afya Nchi nzima’’ Alisema.
Pia Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bw Laurean
Bwanakunu Alimshukuru Mh Rais Magufuli kwa kuongeza Bajeti ya Bohari ya Dawa ,Pia alizungumzia magari hayo
yana jumla ya thamani ya sh Bilion 20.7na kusisitiza msaada huo kutoka Global
Fund hauna masharti yoyote.
Mwaka huu wa Fedha MSD imefanikiwa kuuza madawa yenye thamani
ya sh Bilioni 8,pamoja na uzinduzi huu
Serikali ya Zanzibar imekubali kununua Dawa kutoka Bohari ya Dawa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni