Mkuu wa wilaya Temeke mhe: Felix Lyaniva amewaasa waumini wa dini ya Kiislamu kuepuka migogoro na badala yake waimarishe umoja na udugu ili kuweza kudumisha amani iliyopo katika nchi yetu. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu wa madrassa mbalimbali zilizopo katika wilaya Temeke, katika mkutano ulioandaliwa na baraza la waislamu Tanzania(BAKWATA) wilaya Temeke uliofanyika katika Chuo cha Ualimu (DUCE).
Walimu wa Madrassa waliohudhuria kikao hicho
Aidha katika Hadhara hiyo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es salaam Sheikh Alhadi Musa Salim amesema na kuwaasa waumini wa kiislamu na viongozi wake kufuata kauli mbiu ya ya Baraza la waislamu Tanzania (BAKWATA) inayosema Walimu Tujitambue Tubadilike Tuache Mazoea. ili kuweza kutengeneza jamii yenye maadili mema na uadilifu kwa jamii ya kiislamu na Mkoa kiujumla. Vilevile aliwasisitiza walimu wa madrassa kuwafundisha wanafunzi wao yaliyo mema na kutengeneza mtaala mmoja wa kufundishia masomo ya dini ya kiislamu.
Sheikh Mkuu wa Mkoa Wa Dsm Alhadi Musa Salim.
Pamoja hayo wananchi wa wilaya Temeke wanatakiwa kudumisha ulinzi na usalama wa wilaya yao kwani jamii yoyote yenye amani na utulivu ndio huchochea maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni