Timu ya wataalamu kutoka
Halmashauri ikiongozwa na mratibu wa mradi Bw. Edward Simon pamoja na washauri
kutoka taasisi mbalimbali na Viongozi wa Serikali za Mitaa wapitia michoro ya
barabara na masoko ili kulinganisha na hali halisi ya maeneo yanayohitaji huduma ya haraka.
Huduma hizo ni pamoja na barabara
na madaraja ambapo kwa sasa kumekuwa na
changamoto ya vivuko na ubovu
miundombinu unaopelekea ucheleweshwaji wa shughuli za kimaendeleo kutokana na
kutofikika kwa urahisi, Ubovu huo hupelekea wagonjwa wengi kupoteza maisha ama kufika katika vituo vya Afya wakiwa katika hali mbaya.
Maeneo husika yatakayopitiwa na mradi huu ni pamoja na Soko la Mtoni Mtongani na Barabara ya TRH, Aljazira,
Muungano, Klinic, Kizinga, Ndibalema na Bugdadi.
WATAALAMU WAKIWA KATIKA MAJADILIANO
ENEO LA SOKO
BARABARA YA TRH
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni