Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva aongea na
wafanyabiashara wa Tandika na kuwaahidi kutatua kero zinazowapata pindi wawapo
katika biashara zao. Aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea maeneo
yanayotoa huduma za jamii katika wilaya ya Temeke. Lyaniva aliwaambia
wafanyabiashara hao kuwa ataondoa kero zote zinazolikumba soko hilo . Moja ya
kero kubwa inayoikumba soko hilo ni miundo mbinu inayoizunguka soko hilo,
ikiwemo kutuama kwa maji kipindi cha mvua. Lyaniva awaahidi kuwa atashughulikia
kero hizo ili kuhakikisha mahali hapo panakua salama kwaajili ya kutoa huduma za
kijamii.
Katika ziara hiyo aliambatana na katibu Tawala wilaya,watumishi
kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,diwani wa
Tandika,wenyeviti wa Mitaa,wakuu wa vyama vya siasa mbalimbali,wajumbe wa Mitaa,afisa
Tarafa Chang'ombe na wadau wa utoaji huduma za jamii mbalimbali ikiwemo TARURA,TAKUKURU,DAWASCO
na TRA.
Katika hatua ingine mkuu wa wilaya alielekea ofisi ya kata ya
Tandika ambapo alifanya kikao cha wadau wa maendeleo na wananchi. Ambapo alisisitiza
kuhakikisha wanafunzi wote waliofauru darasa la saba 2017 kama wameripoti
shuleni. Aliwaasa wazazi kutoa ushirikiano ili watoto wao wasibaki nyumbani
kujiingiza katika makundi hatarishi.
Hata hivyo Lyaniva aliwataka wananchi kutoa kiwango stahiki
cha kuzoa takataka ili kusaidia zoezi la ukusanyaji taka kuwa rahisi. Pia
alisisitiza usafi wa kila jumamosi kwa wananchi wote ni lazima.
Pia aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo ya jamii
inayotolewa na serikali kwa riba nafuu kupitia benki ya DCB. Wakinamama na
vijana wamehamasishwa kwenda kuchangamkia fursa hiyo ili kujikwamua katika hali
ya kiuchumi na jamii.
Lyaniva alisisitiza kuwa rushwa ni adui wa haki hivyo endapo
mwananchi atakutana na mazingira yoyote ya rushwa atoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU
Wilaya ili hatua kali za kisheria zichukuliwe. Alisema huduma za jamii ni bure
kwa kila mtu hivyo wananchi wasiruhusu vitendo vya rushwa. Aidha aliwataka
wananchi kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ili
kuiongezea mapato serikali,na kwa mapato hayo hayo yatasaidia kuboresha huduma
za jamii.
Ziara hiyo ya mkuu wa wilaya yenye lengo la kusikiliza na
kutatua changamoto zilizopo katika jamii itaendelea katika kata zote zilizopo
wilaya ya Temeke katika vipindi tofauti tofauti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni