Mstahiki
Meya wa Baraza la Manispaa ya Mjini Zanzibari Mh; Khatibu Abdulrahman afurahishwa
na juhudi za uwendezeshwaji wa shughuli za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Alisema
hayo wakati wa kuhitimisha mafunzo yaliyodumu ndani ya siku tatu katika ukumbi
wa Iddi Nyundo uliopo Manispaa ya Temeke.
Abdulrahman alionesha
utayari wa kufanya mabadiliko katika halmashauri ya Zanzibari baada ya kupata
mafunzo hayo. Pia aliwapongeza uongozi mzima wa Manispaa ya Temeke kwa jinsi
walivyojipanga kuhakikisha wanawafikia wananchi katika nyanja zote za kijamii.
Mafunzo hayo
ambayo yalifungwa na Mstahiki Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo,alisema
''mafunzo haya yatadumisha ukaribu na mahusiano ya utendaji wa halmashauri zetu hivyo tuendeleze''.
aliwapongeza wageni kwa kuja na kujifunza kwetu, na pia aliwakaribisha wakati
mwingine kuja kujifunza Temeke.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni