Mkuu wa
Wilaya ya Temeke Mh; Felix Lyaniva awataka wadau wa maendeleo Temeke
kuhamasisha ulipaji wa kodi na tozo zinazotozwa na Halmashauri ikiwemo leseni,ushuru
na faini mbalimbali.Aliyasema hayo alipokua akifungua kikao cha kamati ya
ushauri ya Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo katika viwanja
vya Manispaa Temeke.Kikao hicho kilijumuisha wakuu wa idara na vitengo,
watendaji wa kata 23 za Temeke,viongozi wa dini,wawakilishi wa wananchi,
viongozi wa vyama vya siasa mbalimbali,makundi maalumu na wadau mbalimbali wa
maendeleo ya Temeke.
Kikao kilijadiri
mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya
maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019, hivyo wajumbe walipitia na
kutoa mawazo yao katika uboreshwaji wa makisio ya bajeti mpya.
Hata hivyo
Halmashauri ya manispaa ya temeke kwa kupitia wataalamu wake mbalimbali
inatazamia kukusanya zaidi ya Bilioni 32 katika vyanzo vyake vya ndani,ikiwa ni
makisio ya bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Halmashauri
ya Manispaa ya Temeke inatazamia kutumia Sh;Bilioni 15,452,505,000.00 kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo inagusa
jamii kwa ujumla. Miradi inayotazamiwa kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa shule za
msingi na sekondari,ununuzi wa madawati, ujenzi wa zahanati,kujenga miundo
mbinu ya usambazaji maji na ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na wakala wa
barabara TARURA.
Aidha Mkuu
wa Wilaya aliwataka watendaji kusimamia utekelezwaji wa bajeti mpya kwa misingi
ya haki, na kuongeza ubunifu katika kupatikana vyanzo vipya vya mapato.
Lyaniva
aliwakumbusha wajumbe wote kuwa mabalozi wazuri katika nafasi zao za utendaji ili
kumunga mkono Raisi wa nchi Mh;John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuleta
maendeleo ya kijamii ikiwemo sera ya Elimu bure.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni