Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepokea ugeni
kutoka Halmashauri ya kati (Wilaya ya kati) kutoka Zanzibar. Ugeni huo wenye
lengo la kudumisha uhusiano wa halmashuri zote mbili. Ushirikiano huo uliodumu
tangu mwaka 2000 wenye lengo la kuleta maendeleo ya kijamii katika halmashauri
hizo.
Ujio huo uliambatana na watendaji, madiwani na wachezaji kutoka Halmashauri
ya kati Zanzibar. Ugeni huo uliongozwa
na Meya wa Halmashauri ya Zanzibar Mh; Said Mtaji Askari pamoja na Mkuu wa
Wilaya ya Zanzibar.
Katika kusheherekea sikukuu ya Pasaka ilichezwa michezo
mbalimbali katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi. Pia ilichezwa mechi ya
kirafiki ya mpira wa miguu kati ya Madiwani wa Temeke na Madiwani kutoka Halmashauri ya Zanzibar ambayo ilikua kivutio kikubwa kwa watazamaji,ambapo
matokeo yalikua sare kwa magoli 4-4. Pia timu ya wanawake ya mpira wa kikapu ilicheza
ambapo timu ya wanawake ya watumishi ili ongoza kwa magoli yasiyo na idadi.
Kabla ya ufunguzi wa michezo hiyo yalifanyika
mazoezi ya viungo(aerobic) ambayo yalihusisha wanamichezo wote. Ambapo
watumishi wa Temeke walionekana kuwa na nguvu na pumzi kubwa.
Hadi kufikia mwisho wa michezo hiyo hakuna
aliyepata majeraha na michezo ilikwisha salama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni