Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Ndg. Prim Damas kwa kushirikisha
wakuu wa idara na vitengo wafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo katika
Manispaa hii. Katika ziara hiyo
iliyofanyika maeneo ya Kijichi, Mbagala Kuu, Mianzini, Keko,Mibulani, Buza
,Yombo vituka,Sandali na Temeke .
Ziara hiyo ya siku mbili imefanikiwa kupitia maeneo yote ya miradi ya Dar es Salam Metropolitan Development Project ( DMDP) pamoja na ya Manispaa na kujiridhisha na utendaji kazi licha ya changamoto ya mvua inayoendelea katika maeneo mengi hapa Jijini.
Miradi hiyo itawanufaisha
wananchi wa maeneo yanayozunguka miradi hiyo hivyo kuwaondolea changamoto
mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili kabla ya kufikiwa na miradi
hiyo.Amebainisha hayo kaimu mkurugenzi
na kuwataka watumie fursa ya kujipatia ajira kupitia miradi hiyo.
Miradi hiyo ni barabara
,madaraja,vituo vya afya,masoko,vituo vya usafiri , vyumba vya madarasa pamoja
na miradi ya maji safi. Mf. kata ya Sandali barabara ya Mchicha yenye urefu wa
km. 1.8 ambayo imegharim Tsh. 2.7 bilioni pia soko kubwa la kisasa linalojengwa
katika kata ya Kijichi lenye uwezo wa
kubeba wafanyabiashara zaidi ya
300, soko hilo limegharimu kiasi cha Tsh. 352 bilioni pamoja na kituo cha
usafiri kitakachojengwa karibu na soko hilo ili kurahisisha huduma za kijamii.
Aidha katika hatua nyingine Ndg.Damas
amewataka wahandisi kuhakikisha wanamaliza kazi walizopewa kwa wakati ili
wakazi wa maeneo husika wapate kunufaika nazo. Aliongeza kwamba ''hii yote ni
kuhakikisha tunaendana na kasi ya awamu ya tano ya kufikia maendeleo''.
Aliagiza wananchi wote wanufaika
wa miradi hiyo kuhakikisha wanatunza maeneo hayo na miundombinu yote ya miradi
pale ujenzi utakapokamilika na kuhakikisha kodi na tozo zote zinalipwa kwa
wakati.
Huu ni mwendelezo wa ziara ya
Kaimu Mkurugenzi Damas ambayo itahusisha
Madiwani katika siku zijazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni