Timu ya ukaguzi ya
athari zitokanazo na mvua toka Halmashauri ya Manispaa Temeke imetembelea shule
ya Sekondari Kurasini iliyozungukwa na maji kufatia mvua zinazoendelea kunyesha.
Timu hiyo ikiongozwa
na Afisa Elimu Sekondari Ndg:Donald Chavila ilipokelewa na uongozi wa shule imejionea
maji yaliyotuama katika shule hiyo nakukosa mwelekeo baada ya mvua kubwa
kunyesha tangu siku ya Jumamosi.
Baada ya ukaguzi wa
shule timu ilikubaliana kuchua hatua za awali za utoaji maji ili masomo
yaendelee.Hatua za haraka ambazo zimechukuliwa ni pamoja na kumwaga dawa
yakuzuia magonjwa ya mlipuko.Kuzibua na kuongeza kina cha maji katika mtaro wa
awali.Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepanga kuboresha mtaro huo
kwa kuujenga kwa zege.
Katika hatua nyingine
Mkuu wa shule ya Sekondari Kurasini Mwl; Florentina Asanga aliweka wazi tatizo
hilo kujirudia kila msimu wa mvua ufikapo.Hivyo ameupongeza uongozi mzima wa Halmashauri
kupitia Mkurugenzi mtendaji Ndg:Nassibu Mmbaga kwa kuonesha nia ya kutokomeza
tatizo hilo katika shule yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni