Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke Ndugu
Nassibu B Mmbaga amepokea msaada wa vifaa vya michezo toka National
Microfinance Bank (NMB). Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Bib:Christian
Lifiga amesema ''tumekuwa tukiunga jitihada za makamu wa Rais Mh: Samia Suluhu za
mazoezi kwa afya bora hivyo tumenunua vifaa vya michezo ili kuboresha Afya za
wananchi''.
Akishukuru kwa msaada wa Vifaa hivyo Mmbaga
alisema vifaa hivyo vitawasaidia katika michezo ya UMITASHUMTA inayotarajia
kuanza mwezi Aprili mwaka huu. Aliongeza
kupitia utoaji wa vifaa hivi inatupa nguvu kwamba michezo inatuleta pamoja.
Naye afisa elimu Msingi Temeke Bib: Dafroza Ndalichako aliwashukuru NMB kwa kuona umuhimu wa michezo hata kuwakumbuka
Temeke,hata hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za
serikali katika sekta mbalimbali.
Vifaa vilivyotolewa ni jezi za michezo zenye
thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili. Zitasaidia timu za shule
ambazo zitashiriki michezo zitashiriki michezo ya UMITASHUMTA kiwilaya. Ambapo
michezo hiyo kitaifa itachezwa jijini Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni