Katika kuadhimisha siku ya upandaji miti
kitaifa, Manispaa ya Temeke imeitikia kauli hiyo kwa kupanda miti 500 katika
shule ya sekondari ya St.Augustine iliyopo Buza inayomilikiwa na kanisa la
Anglikana Dayosisi ya Dar Es Salaam.
Zoezi hilo ambalo limesimamiwa na mawakala wa
huduma za misitu kutoka kanda ya mashariki
na ngazi ya Wilaya ya Temeke(TFS) kupitia Idara ya Misitu. Pia maadhimisho hayo
yalihudhuria na watendaji wa mtaa,
mwenyekiti wa mtaa wa buza,viongozi wa dini,wananchi na mkuu wa shule wa
St.Augastine pamoja na walimu na
wanafunzi wa shule hiyo.
Sherehe hizo zilipambwa na mgeni rasmi ambaye ni
katibu Tarafa wa Mbagala Bib;Bertha Minga ambaye alimwakilisha Katibu Tawala
wilaya ya Temeke Bwn; Hashim Komba.
Bib;Minga alisisitiza upandaji wa miti katika
makazi ili kuleta mwonekano mzuri wa mazingira. Pia aliwataka wananchi zoezi la
upandaji miti liwe endelevu, ili kurudisha uoto wa asili ambao ulipotea. Minga alisema ''kutunza mazingira ya kwa
kupanda miti ya kutosha ilikurudisha uoto wa asili ambao ulipotea''. Pia alisisitiza misitu sio sehemu ya uhalifu, itunzwe na kutumika vizuri kwa ajili ya
maendeleo ya Tanzania ya viwanda. Aidha Bi;Minga alipanda miti kama ishara ya
kuadhimisha zoezi hilo. Pia aliwapongeza TFS Wilaya ya Temeke kwa jitihada zao
za kupanda miti maeneo mbalimbali ya Temeke.Amewahamasisha wadau wengine
kujitokea na kupanda miti ili kuboresha mazingira asilia ya wilaya hiyo.
Mamlaka ya huduma za misitu(TFS) wilaya ya
Temeke kwa miaka mitatu imeweza kupanda miche 5000 katika maeneo mbalimbali
katika Wilaya ya Temeke. Kwa mwaka 2018 imepanda miche 1200 ikiwemo miche ya matunda.
Sherehe hizi zinaadhimishwa tarehe 1 mwezi wa 4 kila
mwaka ,ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni;
''Tanzania
ya kijani inawezekana tupandeni miti kwa maendeleo ya viwanda''
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni