Kitengo cha Ustawi wa Jamii katika Halmashauri
ya Manispaa ya Temeke kimeamua kuweka mazingira rafiki ya kumkuza mtoto ili
kumhatarisha na majanga mbalimbali yanayojitokeza katika kipindi chote cha
ukuaji.
Matarajio hayo yalijadiliwa katika kikao cha
taarifa ya ulinzi na usalama wa mtoto kilichofanyika katika ukumbi wa Iddi
Nyundo uliopo Manispaa ya Temeke. Kikao hiko kiliudhuriwa na Naibu Meya wa
Manispaa ya Temeke Mh; Rajabu Mkenga wa kata ya Miburani ambaye alikua Mwenyekiti
wa kikao,waheshimiwa madiwani,wakuu wa Idara, maafisa Ustawi wa Jamii,timu ya
ulinzi na usalama ya mtoto,Polisi na Magereza.
kikao hicho kilijadili taarifa ya kitengo cha
ustawi wa jamii kwa mwaka 2017/2018 shughuli zote zilizofanyika, ikiwemo
kuwapatia malezi mbadala watoto 30 waliofanyiwa ukatili,kuwaonganisha watoto 40
na familia zao,kutoa msaada kwa familia 7 zilizopata watoto zaidi ya wawili kwa
mpigo n.k Pia kikao kiliangalia mafanikio na changamoto wazipatazo katika
kitengo.
Alipokua akitoa mafunzo ya namna yakumlinda
mtoto katika jamii yetu,afisa ustawi wa jamii Bib;Lilian Mafole ameitaka jamii
kushirikiana na dawati la familia na watoto ili kuzungumza changamoto
wanazokutana nazo watoto katika jamii nzima.Bib Mafole alisema
''watoto wanachangamoto mbalimbali, ni lazima
sisi tunaowazunguka tuwasikilize ili tuweze kuzitatua''.
Alitaja baadhi ya changamoto wanazokutana nazo
watoto ni pamoja na kulawitiwa na ndugu zao,ndoa za utotoni,makundi hatarishi
n.k. Pia aliwaomba wazazi kutokua chanzo cha kuharibu watoto kwa kuendeleza
migogoro katika familia.
Pia aliwaomba madiwani kusaidia kutoa elimu kwa
wananchi juu ya malezi bora katika ngazi ya familia na jamii ili kupunguza
matukio ya ukatili na vitendo vya unyanyasaji wa watoto.
Katika hatua ingine afisa ustawi Bib;Saraha
Nzelwa alitoa elimu ya mfumo wa
DHIS2(District Health Informationn System) ambao kwa sasa unatumika kwaajili ya
ukusanyaji na kutunza taarifa za watoto waliofanyiwa ukatili na unyanyasaji
,wanaokinzana na sheria na walio kwenye hatari ya kukinzana na sheria. Mfumo
huo umekua ukirahisisha upatikanaji wa takwimu za watoto katika Manispaa ya
Temeke. Papohapo mtaalam mwezeshaji kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)
Bib;Happy Nyanda aliwapitisha madiwani katika mfumo huo, nakuonesha kiuhalisia
namna unavyofanya kazi.
Aidha Mh;Mkenga aliwashukuru kwa mafunzo ambayo
wameyapata katika kikao hicho,pia aliwapongeza kwa dhati kitengo cha ustawi wa
jamii kwa namna wanavyofanya kazi kubwa yakufatilia mienendo ya ukuaji wa
watoto katika jamii pamoja na kuchimbua matatizo wanayokumbana nayo watoto
katika makuzi yao.Aliahidi kuungana nao ili kuweza kutatua changamoto ambazo
zinajitokeza ikiwemo upungufu wa bajeti.Hivyo amewataka wazazi kutokukimbia
majukumu yao ya kuhudumia na kulea watoto.Ameitaka jamii kutoa ushirikiano
wakutosha kwa vyombo husika ili kufichua maovu yote na ukatili unaofanywa kwa
watoto.
Dawati la familia na watoto linatekeleza
shughuli za watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama
UNICEF,JSI,PACT,Baba watoto,WEI,WLAC,YCRC,Salvation Army,Pasada,
Compassion,sekta za kiserikali mfano,Madawati ya jinsia,polisi,makao ya watotot
ya watu binafsi,hosptali,maendeleo ya jamii,elimu msingi na
sekondari,magereza,mahakama na huduma kwa jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni