Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 30 Aprili 2018

TEMEKE KUTOA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WASICHANA 6,721


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Felix Lyaniva afanya uzinduzi utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi katika shule ya sekondari Charambe ambapo zaidi ya watoto 40 wamechanjwa.


Chanjo hii itachanjwa kwa watoto wenye umri wa miaka 14 kwa awamu ya kwanza, ambapo mpango wa kuwachanja mabinti wote wa kuanzia umri wa 9-14 itafanyika kwa mwaka 2019.

Uzinduzi huo uliudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo diwani wa kata ya Mianzini Mh:Abdallah Kipende,wataalam kutoka Wizara ya Afya,wataalam wa Afya kutoka Manispaa,kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Temeke pamoja na viongozi wa dini.

Lyaniva alitoa shukrani zake kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake za kuleta mabadiliko katika sekta ya afya hususani afya za akina mama.Alisema '' serikali imetumia gharama kubwa kutoa chanjo hii hivyo wazazi,walezi na jamii nzima tuhakikishe wasichana wenye umri wa miaka 14 wanapata chanjo kwa awamu zote mbili bila kukosa''.

Lyaniva aliongeza chanjo hii itapunguza wimbi la maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi katika taifa letu hivyo wazazi msipuuze.

Akitoa somo kwa wanafunzi hao juu ya saratani,mwakilishi kutoka Wizara ya afya Bi. Zuhra Mkwizu aliwataka wanafunzi wasiwe na hofu kwani chanjo hiyo ni salama na haina madhara kabisa.

Alisisitiza kwamba Chanjo hii imethibitishwa kitaifa na  kimataifa na  imethibitishwa na shirika la afya Duniani (WHO).
"Chanjo hii ni salama na haina madhara kabisa hivyo kuwataka baada ya miezi sita kurudia chanjo ya pili ili kukamilisha dozi kamili"

Nao viongozi wa dini walipata wasaa wa kuwausia watoto hao, namna ya kujilinda na kujichunga dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kuepuka ngono zembe,kuacha tamaa.Huku wakitolea mifano katika vitabu vitakatifu jinsi vinavyokataza kuacha anasa na dhambi.

Chanjo hii ilizinduliwa na Makamu wa Rais kitaifa katika viwanja vya Mbaragala Rangi tatu na kwa sasa inaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika Wilaya  ya Temeke chanjo hii itatolewa katika vituo 274,ambapo vituo 197 ni mashuleni na vituo 77 ni katika vituo vya afya.Takribani wasichana 6,721 wanatarajiwa kupata chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi.Ambao itajumuisha idadi ya wale waliopo mashuleni na nyumbani.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...