Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 10 Aprili 2018

CHANJO YA SARATANI YA KIZAZI BURE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuanzia sasa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi itatolewa burea.




Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akizindua chanjo ya Saratani ya Shingo ya kizazi kitaifa katika viwanja vya Zakhiem Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.






Mama Samia amebainisha kuwa Serikali inapambana kuhakikisha Afya ya mwananchi inalindwa na kuwawezesha wananchi kuwa na afya njema itakayowasaidia kuwa na nguvu ya uzalishajimali ili kufikia uchumi wa viwanda.







Pamoja na hayo aliwataka Wazazi kutokuwa na hofu juu ya chanjo hii kwani ni salama na haina madhara yoyote ya kiafya




"Wakina mama, naomba mfahamu kuwa chanjo hii imefanyiwa utafiti wa ndani na nje ya nchi hivyo haina madhara kwa afya zenu" amesema makamu wa Rais

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewapongeza wadau wa Maendeleo wa Jiji la Dar es Salaam kwa juhudi zao za kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za jamii lakini pia kuitambua kampeni ya ''Afya yangu Mtaji wangu'’.

Akizungumza katika zoezi hilo,Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Wazee Jinsia na Watoto Dr. Ummy Mwalimu amesema'' kwa mwaka 2018 wameanza kwakutoa chanjo hiyo kwa watoto wenye umri wa miaka 14 na kuanzia mwakani wataongeza dozi hiyo hivyo kuanza kuwachanja watoto wa kuanzia miaka 9''.

Dkt. Ummy amevitaja visababishi vya saratani hiyo kuwa ni virusi vijulikanavyo kitaalamu kama Human Papiloma Virus (HPV) ambacho kinaua wanawake wengi katika nchi zinazo endelea na kuambukizwa kwa njia ya ngono.

"Ndugu zangu wakina mama mnapoona dalili yakutokwa na uchafu au damu katika sehemu za siri au kuingia katika hedhi bila mpangilio maalumu ni vema ukachukua hatua za haraka kwa kuwaona wataalam wa afya" amenukuliwa Dkt. Ummy.

Ummy amesema tafiti zinaonyesha kila wanawake 4 wanaoshiriki ngono 3 wanapata maambukizi ya HPV wakati fulani wa maisha yao hivyo jukumu inalo chukua Serikali kwa sasa ni kupambana kwa kutoa chanjo kwa waschana wenye umri mdogo ili kuepusha maambukizi katika umri mdogo.

Katika zoezi hilo lilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh:Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh:Felix Lyaniva na wageni mbalimbali. ambao kwa pamoja kila mmoja kwa nafasi yake alioneka kuwahimiza wananchi kujitokeza katika zoezi hilo na mengine yanayo husu afya zao.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE APOKEA MAPIPA ZAIDI YA 241 KWA AJILI YA KAMPENI YA “TEMEKE BILA UCHAFU INAWEZEKANA” Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh F...