Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mh.Kate Kamba pamoja na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi wafanya ziara Manispaa ya Temeke na kukagua miradi ya maendeleo pamoja na ukaguzi wa utekelezaji wa Chama Cha Mapinduzi na kuwakumbusha wajumbe wa chama hicho kimeelekeza serikali kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto zote zinazowakabili wananchi. Katika ziara yake ndani ya Manispaa ya Temeke, amepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya mwaka 2015-2020 iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Felix Lyaniva alisema ''Tunaendelea kutekeleza ilani ya Chama Chetu kwa kuhakikisha tunawafikia Wananchi katika nyanja zote za maendeleo kwa ukaribu zaidi''.
Kuhusu utatuzi wa kero za wananchi Mh. Lyaniva amesema wilaya inaendelea kutatua kero mbalimbali za wananchi hivyo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kero za wananchi. Pamoja na hayo kumeanzishwa dawati la kushughulikia kero hizo za Manispaa ambapo imeongeza saa moja zaidi baada ya muda wa kazi ili kuwafikia Wananchi wenye matatizo kwa ukaribu zaidi. Ili kuhakikisha Wananchi wanatatuliwa matatizo yanayowakabili kwa haraka ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeanzisha utaratibu wa kusikiliza kero za Wananchi kwa kata kila baada ya miezi mitatu.
Aidha Mh. Lyaniva ameelezea mradi wa maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam (Dar es salaam Metropolitan Development Project-DMDP) kuwa Temeke ni miongoni mwa Halmashauri zinazotekeleza mradi huo kwa Mkopo toka benki ya Dunia na kusimamiwa moja kwa moja na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Akifafanua kuhusu Utekelezaji wa ilani ya CCM aliwaeleza wajumbe kuwa Halmashauri imechangia TZS 20.3Bilioni kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wanaopisha ujenzi wa miundombinu ya Mradi huo. Alisema ''Mradi wa DMDP ni miongoni mwa miradi ya kimkakati ambayo lengo lake ni kuboresha miundombinu mbalimbali ya Jiji letu''.
Katika ziara yake Mwenyekiti huyo ametembelea miradi mbalimbali na kuelezwa kuhusu miradi ya Ujenzi wa Masoko sita ya kisasa na vituo vya mabasi vitano, ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji ya mvua yenye urefu wa zaidi ya 8.5km, uwekaji wa taa katika mitaa yote inayoguswa na mradi, Ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata ya Buza, Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa kisasa katika Kata ya Makangarawe, Ujenzi wa Barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya Kilometa 95 pamoja na kuboresha mfumo wa ukusanyaji Taka Ngumu.
Katika kukamilisha ziara hiyo Mh Kamba alitoa shukrani kwa Wilaya kwa utendaji na ufanisi katika Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Huku akiisifia Manispaa ya Temeke kuwa wamejitahidi kuweka wilaya hiyo katika hali ya usafi na kuwataka kuendeleza juhudi na kutoa Elimu kwa Umma kuhusu masuala yote ya Usafi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni