JUKWAA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI TEMEKE
LAUNDWA
Katibu
Tawala Wilaya ya Temeke Bw:Hashimu Komba aunda jukwaa la wanawake wajasiliamali
wa wilaya ya Temeke ambao walijitokeza kwa wingi kutoka kata zote za wilaya
hiyo. Akiongea na wanawake hao wajasiliamali leo katika ukumbi wa Iddi Nyundo
Manispaa ya Temeke.
Pichani Bw:Hashimu Komba, Katibu Tawala Wilaya ya Temeke.
kauli mbiu ya kikao hicho ni “Mwanamke tumia fursa kuimalisha uchumi wa
viwanda” ambapo Katibu tawala huyo ameungana na juhudi za Makamu wa Rais Mama
Samia Suluhu ikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa jukwaa la wanawake katika
kuinua uchumi wa mwanamke ili kuleta Maendeleo ya taifa kiwilaya.
Kauli mbiu hiyo ilisemwa na Makamu wa Rais katika siku ya uzinduzi wa Jukwaa la
uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kimkoa lililofanyika katika viwanja vya Posta,kijtonyama.
Ambapo uzinduzi huo ni wa 23,lililoandaliwa na Baraza la uwezeshaji kwa
ufadhili wa benki ya CRDB.
Komba aliwamwagia sifa wanawake kwa juhudi zao za kujikwamua kiuchumi katika
jamii,aliwapongeza akina mama kwanamna wanavyojituma na kuwa waaminifu na kuwa
na uwezo wa kusimamia vipato vyao vidogo wanavyopata kwa kujileta maendeleo
makubwa.
Pichani watumishi wa Manispaa na wanawake wajasiliamali wakimsikiliza Bw:DAS kwa makini.
Ahadi kuwa jukwaa
hilo punde litakopo undwa litakuwa na tija kubwa katika kujitangazia biashara
na ubunifu wa kazi zao wanazofanya katika ngazi za kimataifa,kitaifa,kimkoa,kiwilaya
mpaka kata. Pia watapata fursa mbalimbali za kupiga hatua kama kushiriki
maonesho ya kibiashara ya sabasaba na nanenane. Hivyo asisitiza kuchaguliwa kwa
viongozi walio na uwezo wakusimamia mawazo,ubunifu na ujuzi wa kazi zao ili
kusimamia jukwaa hilo katika kujiletea maendeleo.
Hata hivyo amewapa
moyo kuwa kuelekea katika sera ya uchumi wa viwanda kwa kuanzia waendelea
kutumia technolojia hizo hizo ndogondogo wanazotumia nyumbani kuzalisha bidhaa
mbalimbali ikiwa ni mfano wa viwanda vidogovidogo,wakati wanajiandaa kupata
viwanda vikubwa. Kwakufanya hivyo watakuwa wanajiingizia kipato,pia kuinua
uchumi wa viwanda katika nchi yetu.
Wanawake wajasiliamali wakiwa katika kikao cha uundaji wa jukwaa la wanawake wajasiliamali kiwilaya.
Katika kikao hicho
katibu Tawala huyo alipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
inayoongozwa na John Bwana kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwatambua
wajasiliamali hao ambao wamejitokeza kwa wingi na shauku kubwa kuunda jukwaa
hilo.
Jukwaa hilo
linatazamiwa kuzinduliwa hivi karibuni lengo kuu ikiwa ni kumwinua mwanamke
kufikia katika uchumi wa kati, ambapo inasemekana mwanamke ni mlezi wa familia
na jamii, ukimwezesha mwanamke imeliwezesha taifa.